Diamond na Jux wakutanisha pamoja wasanii zaidi ya watano

Diamond na Jux wakutanisha pamoja wasanii zaidi ya watano

Imekuwa kawaida kwa baadhi ya mashabiki kutoa lawama kwa wasanii kuhusiana na ubora wa video wanazotoa huku wengi wakilalamika kuwa mara nyingi audio zinakuwa nzuri lakini ikija upande wa video wasanii wanaharibu. Japo kutokana na malalamiko hayo wasanii wamekuwa wakiwarushia lawama waongozaji wa video (Directors).

Ni wazi kuwa wimbo wa #Enjoy wa mwanamuziki Jux ambao amemshirikisha Diamond bado unaendelea kusumbua masikioni mwa wapenzi wa burudani huku video ya wimbo huo ikiwa imeachiwa siku ya leo, ndani ikiwa na ubunifu wa kutosha kutoka kwa wakali hao.

Ukiangalia kwa haraka unaweza kuchukulia poa kilichofanyika kwenye video hiyo, lakini ukweli ni kwamba kuna vitu vimeleta utofauti kwenye wimbo huo hasa ukiangalia katika video hiyo utakutana na sura mbalimbali za wakali wa muziki kutoka #Bongo jambo ambalo wengi hawakutegemea kama linaweza kutokea kwenye video ya wimbo huo.

Imezoeleka kwenye vichupa vya nyimbo nyingi huwa vinahusisha wasanii tu waliosikika ndani na video vixen au king kama watahitajika, upekee wa #Enjoy umekutanisha vichwa tofauti humo ndani , ukiachana na ukali wa ngoma yenyewe lakini pia ubunifu uliofanyika unaweza kuwa ni sababu ya wimbo huo kwenda zaidi kwenye mtandao wa #YouTube.

Ukipata nafasi ya kupita au kuangalia kwa umakini utakutana na sura ya wakali kama vile @whozu_ , @rayvanny , @ommydimpoz , @moni_centrozone , @iamlavalava , na @s2kizzy ,  tofauti na watu hao maarufu pia wametumika watu wa kila rika kuanzia watoto hadi wazee jambo ambalo litazidi kuvutia zaidi watazamaji wa kila aina  huku quality nayo ikiwa imezingatiwa.

Tuambie wewe kitu gani kimekuvutia zaidi kwenye video ya Enjoy?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags