Diamond: Manara hakupaswa kufungiwa hadi leo

Diamond: Manara hakupaswa kufungiwa hadi leo

Nyota wa muziki nchini Diamondplatnumz wakati akizungumza kwenye sherehe ya aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara ya kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa , na kumvisha pete mchumba wake Zaylissa, amesema kuwa hadi leo Haji hakupaswa kuwa amefungiwa.

Diamond amesema yeye ni miongoni mwa watu ambao wanamfuatilia sana Haji, lakini kwenye sekeseke lake la kufungiwa hata kama aliteleza, alipaswa awe amefunguliwa muda mrefu, kutokana na mchango wake nchini kwenye upande wa mpira wa miguu.

Mwaka 2022 kamati ya maadili ya TFF ilimfungia Manara miaka miwili kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi na kulipa faini ya Sh20 milioni, kwa kosa la kumtolea maneno yasiyofaa Rais wa TFF Wallace Karia katika mechi ya fainali ya kombe la Azam iliyopigwa jijini Arusha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags