Diamond aweka rekodi tuzo za Grammy

Diamond aweka rekodi tuzo za Grammy

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameweka rekodi nyingine baada ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kutumbuiza katika jukwaa la mfululizo wa vipindi Global Spin vinavyoandaliwa na waandaji wa tuzo za Grammy.

Onesho lake limeoneshwa usiku wa Februari 7, 2022 kupitia mitandao rasmi ya Grammy ambapo Diamond aliimba wimbo wake mpya unaoitwa Gidi pamoja na bendi na wanamitindo ambao kwa pamoja walinogesha onesho hilo.

Kwa onesho lake hilo Diamond anakuwa si tu msanii pekee kutoka Tanzania kupewa heshima hiyo bali ni kwa Afrika Mashariki yote.

Bosi huyo wa lebo ya WCB hajawahi kupata uteuzi wa Grammy lakini kutokana onesho hilo alilofanya ni wazi kuwa ni njia nzuri ya kuweza kuwakilisha nchi katika tuzo zijazo za 64 za kila mwaka za Grammy.

Maonesho haya ya Global Spin, yalizinduliwa mwaka 2021 ambapo huangazia na kushirikisha wasanii kutoka pande zote ulimwenguni.

Kila kipindi kinachorushwa huusisha onesho kutoka kwa msanii au kikundi maarufu kusheherekea ubunifu na nchi zao.

Mfululizo wa kipindi hicho hurushwa kila inapofika siku ya jumanne na ni mara moja kwa wiki kupitia mitandao rasmi ya Grammy ambayo ni YouTube, Facebook, Instagram, na Twitter.                    

Global Spin inalenga kuwaweka mashabiki wa muziki duniani pamoja kwa njia ya kusisimua zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags