Diamond ashika namba 1 Tanzania

Diamond Ashika Namba 1 Tanzania

Msanii wa muziki nchini Tanzania, Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ametajwa kuwa msanii namba moja Tanzania aliyesikilizwa zaidi katika mtandao wa Spotify kwa mwaka huu.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mkuu wa Kitengo cha Digital WCB Wasafi, Kimkayndo ameandiuka kuwa Diamond ndio msanii namba moja aliyetazamwa mwaka huu hivyo anawashukuru mashabiki wote wanaoendelea kumsapoti.

“Diamond ametajwa na Spotify kuwa msanii namba moja aliyesikilizwa zaidi Tanzania kupitia mtandao wao mwaka huu 2021, asanteni kwa kuendelea kutufanya namba moja wa muda wote, makubwa zaidi yanakuja,” aliandika Kimkayndo

 

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post