Diamond arudia nguo, Alivaa miaka minne iliyopita

Diamond arudia nguo, Alivaa miaka minne iliyopita

Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka nchini #DiamondPlatnumz ameweka wazi kuwa koti alilolivaa katika wimbo wake ‘Tetema’ ndilo hilo hilo alilolivaa kwenye wimbo wa Komando alioshirikishwa na G Nako.

Diamond kupitia InstaStory yake ameandika kuwa,

 “Nikuibie siri tu kuwa koti nililovaa kwenye ‘Komando’ ndiyo koti lile lile nililovaa zamani kwenye video ya ‘Tetema’, hii inaitwa utunzaji na kuheshimu mali, kiufupi kutotumia hela hovyo”

Video hiyo ya 'Komando' imeachiwa jana kwenye digital platform za msanii G Nako, hadi sasa tayari imefika number one trending YouTube. Huku video ya Tetema ilitoka miaka minne iliyopita na hadi sasa imefikisha watazamaji zaidi ya  milioni 77 kwenye mtandao wa YouTube.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags