Diamond ajitosa anga za kina Bill Gates

Diamond ajitosa anga za kina Bill Gates

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' amewekawazi kuwa ndoto yake kubwa kwa sasa ni kuwa tajiri namba moja duniani huku akiweka ahadi ya kuwa mtanzania wa kwanza kufikia levo hiyo.

Diamond ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo Septemba 4, 2024 katika uzinduzi wa Wasafi Festival.
Ndoton hizo zinamfanya Diamond aanze kuwaza kupambana kuzifikia ‘levo’ za watu matajiri duniani akiwemo; Elon Musk, Bernard Arnault , Bill Gates, Aliko Dangote na Jeff Bezos.

“Ndoto yangu kubwa katika maisha ni kuwa tajiri namba moja duniani, ndiyo ndoto yangu na ninakuthibitishia kwamba nitakuwa tajiri namba moja duniani, katika moja ya Wasafi Festival kuna shule flani niliwaambia nitanunua siku moja Rolls-Royce na iko imekaa pale inagalagala inapigwa na jua.

"Kwa sababu kwangu mimi naamini kila kitu kinawezekana na nawahakikishia kuwa nitakuwa mtanzania nitakayewakilisha taifa kuwa tajiri namba moja duniani” amesema Diamond

Mbali na hayo ameweka wazi kuwa kabla ya mwaka kuisha amepanga kufungua biashara yake nyingine ambayo itakuwa ikigombaniwa.
Kwa sasa tajiri namba moja duniani ni Elon Musk anayedaiwa kumiliki zaidi ya dola 248 bilioni akifuatiwa na Jeff Bezos mwenye utajiri wa dola 196 bilioni huku namba tatu ikishikwa na Mfaransa Bernard Arnault akiwa na utajiri wa dola 190 bilioni.

Hata hivyo tamasha hilo ambalo linafanyika kila mwaka la Wasafi Festival linatarajiwa kuanza rasmi September 14, 2024 Ruangwa mkoani Mtwara, huku wasanii mbalimbali walijitokeza katika uzinduzi huo akiwemo Barnaba, Chino Kidd, Lava Lava, Mbosso, Abigail Chams, Appy na wengineo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags