Diamond afichua siri ya kufanya kazi na Koffi

Diamond afichua siri ya kufanya kazi na Koffi

Si mara ya kwanza msanii Diamond kuonekana katika wimbo mmoja na mkali kutoka nchini Congo, Koffi Olomide, miaka miwili iliyopita wawili hao walifanya wimbo walioupa jina la ‘waah’ ambao mpaka sasa una zaidi ya viwes million 140 kwenye mtandao wa YouTube.

Kwa mara nyingine tena wawili hao wameonekana tena katika wimbo wao mpya wa ‘Achii’ wenye views 952 ukiwa na saa 20 tuu tangu wa uachie wimbo huo.

Diamond amefichua siri ya kufanya kazi na Koffi akieleza kuwa toka akiwa mdogo amekuwa akitizama miziki ya Koffi na alikuwa mmoja wa shabiki yake mkubwa.

Alimalizia kwa kumshukuru Olomide kwa namna ambavyo anajitoa asilimia mia kuhakikisha wanapata wimbo ambao utawapa raha mashabiki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags