De Gea kuonekana tena Man United

De Gea kuonekana tena Man United

‘Klabu’ ya #ManchesterUnited, inadaiwa kuwa na mpango wa kumrejesha ‘goli kipa’ David de Gea katika kikosi chao, ikiwa ni miezi sita tangu aondoke katika ‘timu’ hiyo.

Kwa mujibu wa Sky Spot News imeeleza kuwa ‘klabu’ hiyo imefikia uamuzi  huo kufuatia wasiwasi kuwa ‘goli kipa’ wao #AndreOnana anaweza kukosekana katika michezo mingi muhimu pindi atakapokwenda kujiunga na ‘Timu’ ya Taifa Cameroon kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), inayoanza mwezi Januari 2024.

De Gea ameitumikia Man United kwa miaka 12, amekuwa mchezaji huru tangu aondoke ‘klabuni’ hapo baada ya kushindwana na ‘klabu’ hiyo iliyolazimika kumpunguzia mshahara ‘kipa’ huyo mwenye miaka 32 ili kusalia ‘klabuni’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags