Dawa nyingine ya kikohozi yaua watoto 18, India

Dawa nyingine ya kikohozi yaua watoto 18, India

Taarifa kutokea Uzbekistan zinaeleza kuwa dawa ya kikohozi aina ya Doc-1 Max iliyotengenezwa nchini India inahusishwa na vifo vya watoto 18 vilivyotokea hivi karibuni nchini humo.

Wizara ya afya ya Uzbekistan imesema kuwa watoto hao walipoteza maisha kutokana na changamoto za kiafya zilizowapata baada ya kunywa dawa hiyo iliyotengenezwa na Kampuni ya Marion Biotech.

Matukio haya yanakuja miezi michache baada ya watoto 70 kufariki nchini Gambia ndani ya miezi michache kutokana na matumizi ya dawa kadhaa za mafua na Kikohozi.

Vilevile, takribani watu 199 wengi wao wakiwa ni watoto walifariki nchini Indonesia ndani ya miezi minne kwa kile kilichotajwa na wataalamu kuwa ni matumizi ya dawa za mafua na kikohozi.

Aidha dawa zote zinazohusishwa na vifo hivi zimetengenezwa nchini India na kwa sasa zimeondolewa kwenye maduka yote katika nchi zilizoathirika.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags