Davido: Ningekutana na mke wangu kipindi hiki nisingemuoa

Davido: Ningekutana na mke wangu kipindi hiki nisingemuoa

Mwanamuziki wa Afrobeat kutoka nchini Nigeria, #Davido ameweka wazi kuwa alikutana na mke wake, #ChiomaAdeleke kabla ya kuwa na pesa wala umaarufu.

Kupitia mahojiano yake hivi karibuni na moja ya chombo cha habari, Davido alisema alikutana na mama watoto wake akiwa anajitafuta na kama angekutana naye kipindi akiwa na pesa basi ingekuwa vigumu kumuoa kwa sababu angehisi kama amempendea mali.

Hata hivyo mwanamuziki huyo alieleza kuwa anafuraha kuzungukwa na watu ambao wanamfahamu kabla ya kupata umaarufu na utajiri. Davido na mkewe walikutana mwaka 2013 na walifunga ndoa ya kimila mwaka jana.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags