Davido na Chioma wasepa Nigeria

Davido na Chioma wasepa Nigeria

Baada ya mwanamuziki Davido kufunga ndoa na mkewe Chioma siku ya Jumanne Juni 25, 2024 na kutiki mji kufuatia na sherehe yao kuzungumzia ndani na nje ya Afrika, wanandoa hao wapya wameripotiwa kuondoka Nigeria kwa ajili ya kwenda Honeymoon.

Kupitia video inayosambaa mtandaoni imewaonesha wawili hao alfajiri ya kuamkia leo wakipanda katika ndege binafsi huku safari hiyo ikidaiwa kuwa ni ya kwenda fungate lakini mpaka sasa haijawekwa wazi ni nchi gani haswa wamekwenda kwa ajili ya tukio hilo.

Ndoa ya Davido na Chioma ilizua gumzo kupitia mitandao ya kijamii baada ya wawili hao kuwa katika mahusiano kwa muda mrefu huku baadhi ya wanawake wakimpongeza Chioma kwa uvumilivu aliouonesha mpaka kufunga pingu za maisha.

Utakumbuka kuwa wawili hao walianza mahusiano ya kimapenzi mwaka 2013 na kuchumbiana mwaka 2019 jijini London.

Davido na Chioma wakati wa uchumba wao walibahatika kupata mtoto wa kiume aitwaye Ifeanyi ambaye alifariki mwaka jana baada ya kuzama kwenye bwana la kuogelea lililopo nyumbani kwako, na kufanikiwa kupata tena watoto mapacha Oktoba, 2023.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags