Davido na Chioma wadaiwa kufunga ndoa

Davido na Chioma wadaiwa kufunga ndoa

Hellow! Bwana weeee! Niaje mko pouwa watu wangu wa nguvu, kama kawaida weekend tunaimaliza kwa yale mastori makubwa yaliotrend kupitia mitandao ya kijamii, basi bwana,

Kati ya vitu vilivyoripotiwa wiki hii ni pamoja na tetesi kuwa staa wa muziki nchini Nigeria, Davido na mpenzi wake, Chioma wamefunga ndoa ya kitamaduni kwa siri. Haya yanajiri wiki chache baada ya wanandoa hao kumpoteza mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu, Ifeanyi ambaye alizama kwenye swimming pool katika jumba la kifahari la msanii huyo katika kisiwa cha Banana, huko Lagos.

Harusi hiyo ya kitamaduni inasemekana ilihudhuriwa na familia na marafiki wachache na za kunyapia ni kwamba harusi inadhaniwa kufanyika tarehe 6 Novemba katika nyumba ya babake Davido, bila kamera kuruhusiwa na mahari ya Chioma ikiwa imelipwa kikamilifu kama inavyotakiwa.

Hata hivyo, kama ndoa hiyo kweli ilifanyika, ilikuwa ni lazima ifungwe ili mtoto wao Ifeanyi ambaye alifariki aweze kuzikwa kama mmoja wa familia ya Davido kulingana na tamaduni za jamii ya Igbo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags