Davido kutoa msaada kwa wenye uhitaji

Davido kutoa msaada kwa wenye uhitaji

Mkali wa Afrobeat kutoka nchini #Nigeria, #Davido ametangaza kuwa atachangia Naira milioni 300 ambazo ni sawa na tsh 500 milioni kwenye vituo vya watoto yatima vilivyopo nchini Nigeria.

Hii siyo mara ya kwanza kwa Davido kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji, mwaka 2021, kupitia ukursa wake wa X (zamani Twitter) alituma ujumbe wa kuomba pesa kwa mashabiki zake kwa jili ya kukomboa gari yake ya ‘Rolls Roys’,  lengo likiwa ni kupata pesa ya kuwasaidia watu wenye uhitaji ambapo alipata tsh 300 milioni, huku mwenyewe akiongezea tsh 20 milioni.

Aidha muendelezo wa matukio hayo ya kuomba fedha imemuwezesha mwanamuziki huyo kufungua Taasisi yake ya kutoa misaada kwa watu wenye mahitaji, ijulikanayo kwa jina ‘David Adeleke Foundation’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags