Davido atumia zaidi ya tsh 200 milioni kununua mikoba ya mkewe

Davido atumia zaidi ya tsh 200 milioni kununua mikoba ya mkewe

Msanii kutoka nchini Nigeria, Davido amewashangaza wengi baada ya kutumia kiasi kikubwa cha pesa kununulia pochi kwa ajili ya mkewe.

Davido anadaiwa kutumia zaidi ya tsh 250 milioni kwa ajili ya kumzawadia mkewe ambapo amenunua pochi hizo za kampuni tofauti tofauti kama zawadi ya kumkaribisha mkewe nyumbani baada ya kutoka hospitali kujifungua watoto mapacha.

Licha ya kumzawadia mikoba hiyo inadawa msanii huyo alimpatia mkewe mali yenye thamani ya dola 900,000 Atlanta, nchini Marekani kama shukurani yake kwa kumzalia watoto hao mapacha.

Davido na Chioma walifanikiwa kupata watoto wawili mapacha ambapo mmoja ni wa kike na mwingine wa kiume baada ya kumpoteza mtoto wao wa kiume Ifeanyi Adeleke October 2022 baada ya kutumbukia kwenye bwawa la kuogelea.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post