Davido amshitaki mama watoto wake

Davido amshitaki mama watoto wake

Mkali wa Afrobeats kutoka Nigeria, #Davido amemshitaki mama watoto wake aitwaye Sophia Momodu, kwa kwa kudai huduma ya malezi iiliyopitiliza ya binti yake wa kwanza, aitwaye Imade kwa manufaa yake.

Tovuti ya Punch News Paper imeeleza kuwa Davido amemshutumu mwanamke huyo kwa kumtumia binti yao ili kupata manufaa makubwa ya kifedha kutoka kwake, huku akidai kuwa mara zote amekuwa akitaka fedha nyingi, licha ya kutekeleza majukumu yake kwa Imade kama Baba.

Katika kesi hiyo Davido ameeleza kuwa Sophia alikataa nyumba ya Naira milioni 200 ambapo sawa na Sh 350.3 milioni yenye bwawa la kuogelea aliyonunua kwa ajili ya binti yake na kutaka awe anamlipia kodi ya naira milioni 5 sawa Sh 9 milioni kila mwaka.

Katika hati hizo zilizofikishwa mahakamani pia zilieleza kuwa mwanamke huyo alimtaka Davido awe anamlipa mfanyakazi wake wa nyumbani dola 800 sawa na Sh 2.1 milioni kwa mwezi na  dola 19,800  sawa tsh 51.6 milioni kila mwaka kama pesa za matumizi ya mtoto.

Utakumbuka kuwa mwanamuziki huyo ambaye ana watoto sita, wavulana watatu mmoja ambaye sasa ni marehemu, na wasichana watatu huku watoto wawili mapacha akiwapata kutoka kwa mkewe Chioma Rowland.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags