Davido afunguka kutokuwa kwenye mawasiliano mazuri na Burna Boy, Wizkid

Davido afunguka kutokuwa kwenye mawasiliano mazuri na Burna Boy, Wizkid

Mkali wa Afrobeat kutoka nchini Nigeria Davido ameweka wazi kutokuwa na mawasiliano mazuri na baadhi ya wasanii wenzake ambao ni Burna Boy na Wizkid.

Davido ameyasema hayo wakati wa mahojiano yake na podcast ya SWAY ambapo ameeleza kuwa hawasiliani na mastaa hao licha ya kila mmoja kuwa na namba ya mwingine huku akisisitiza kuwa kwa upande wake haoni shida kwani kila mmoja anabarikiwa kwa wakati wake.

Aidha kupitia mahojiano yake hayo ameweka wazi kuwa kwa sasa muziki wa Afrobeat umekuwa na ushindani mzuri kwani kila mmoja amekuwa akipambana kuupeleka muziki huo levo nyingine huku akiwataja baadhi ya mastaa ambao wamekuwa wakifanya vizuri siku za hivi karibuni akiwemo Rema, Ayra Starr pamoja na Kizz Daniel.

Licha ya hayo amefunguka kuja na ‘kolabo’ na mwanamuziki kutoka nchini Marekani Victoria Monet, huku akidai kuwa anamsubiri Rihanna (Riri) baada ya kusema kuwa anaikubali ngoma ya ‘Unavailable’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags