Dan Sur afanya upasuaji kuondoa nywele kichwani

Dan Sur afanya upasuaji kuondoa nywele kichwani

Huku mitandaoni ni gumzo baada ya Rapa kutokea Mexico, Dan Sur kutangaza kufanyiwa upasuaji na kuondolewa nywele zake kichwani na kuwekewa cheni za dhahabu.

Dan Sur anasema alitaka kufanya kitu tofauti, kuwa binadamu wa kwanza kuweka cheni za dhahabu kichwani badala ya nywele.

“Hizi cheni zimewekwa ndani ya ngozi yangu, mimi ni rapa wa kwanza kuwa na cheni za gold kama nywele,” alisema Rapa huyo.

Daktari wa Upasuaji ameongea na Yahoollife na kusema “upasuaji huo ni hatari kufanya, unaruhusu bakteria kuingia katika ubongo na uzito wa hizo cheni sio salama kwa mwili wake,” alisema

Tuambie nawe msomaji wetu hii imekaaje kwako unaweza kumshauri nini msanii kama huyu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags