Daimond na Alikiba waanza Upya vita ya muziki

Daimond na Alikiba waanza Upya vita ya muziki

Kuna nyakati kiwanda cha muziki wa burudani kinapoa hasa msanii DiamondaPlatnumz, na #KingKiba wasipoachia kazi zao, vichwa hivi viwili kwenye ‘gemu’ ya #BongoFleva vimekuwa na amsha amsha ya upinzani kutokana na wingi wa mashabiki wao kama ilivyo kwa #Simba na #Yanga.

Hivi karibuni wawili hawa wamechangamsha ‘gemu’ ya muziki wa #Bongo na kuamsha hisia za mashabiki wao kuwaongelea kwa ushindani.

Vita kati ya #Mondi na #Kiba inachangia kukuza muziki wa #Bongo na ndio maana wawili hawa wakitoa ngoma mashabiki wao huzishindanisha.

Baada ya ukimya wa muda kwa wanamuziki hao, vita mpya ya ushindani imeanza tena baada ya wawili hao kuachia ngoma huku kila mmoja akitaka kukaa namba moja mjini #YouTube.

Vita hiyo inachochewa na idadi ya watazamaji YouTube ambapo wimbo wa Diamond Shu unaongoza kwa watazamaji 1.7M na Alikiba wimbo wa Sumu hadi sasa umefikiwa na watu 1.2M.

Diamond ametolewa namba moja trending ikiwa ni siku ya tano tangu ameachia wimbo huo huku Alikiba akiwa ameshikilia namba mbili ikiwa ni siku ya tatu tangu aachia wimbo huo.

Wimbo wa Sumu, Alikiba ameshirikiana na Marioo ambapo kwa upande wa #Diamond kwenye Shu amemshirikisha Chley. Wakati huo huo wasani hawa kila mmoja aliitumia weekend yake kwa ku-promote kazi zake.

Alikiba alifanya party yake ambayo ilihususha wimbo wa #Sumu na kwa Diamond akiwa na Jux walifanya private party kwaajili ya wimbo wa Jux uitwao #Enjoy ambao #Diamond ameshirikishwa humo ndani, hadi sasa wimbo huo unaendelea kufanya vizuri YouTube na umeshika namba moja.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags