Dada wa kazi amshtaki bosi kwa kutomlipa mshahara miaka 5

Dada wa kazi amshtaki bosi kwa kutomlipa mshahara miaka 5

Msichana wa kazi za ndani (house girl) aliefahamika kwa jina la Zuhura Ramadhani mwenye umri wa miaka 30, amemshtaki bosi wake Khadija Katusi Muoza katika Serikali ya Mtaa ya Mpiji Magohe kwa kutomlipa stahiki zake kwa zaidi ya miaka mitano ambapo kwa mwezi mshahara wake ni Tsh. 35,000.

Zuhura anasema “Nimefanya kazi kwake kwa Miaka 14 kwa wema, nimewalea watoto wake vizuri, ilifikia kipindi nilikuwa natoa Fedha zangu kusaidia familia yake pindi aliposema mambo yake si mazuri na ananihifadhia mishahara yangu, mama yangu anaumwa na ninahitaji kumuuguza” amesema Zuhura

Kwa upande wa bosi Khadija amesema “Kweli ananidai nimeishi naye vizuri na kuna muda alikuwa akitoa Fedha zake kusaidia familia lakini maisha yameyumba, nikipata hela nitamlipa.” Amesema bosi wake huyo

Aidha Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Saidi Diuchile amesema “Khadija amekubali kwa maandishi kuwa atalipa lakini kumekuwa na ugumu kutekeleza, baada ya mvutano amelipa Tsh. 200,000 kati ya zaidi ya Tsh. 2,860,000 ambayo anadaiwa.”

Chanzo Jamii Forums


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post