Dada atapeliwa na Elon Musk feki

Dada atapeliwa na Elon Musk feki

Mwanamke mmoja kutoka nchini Korea Kusini aliyejulikana kwa jina la Jeong Ji-sun, ametapeliwa kiasi cha dola 50,000 ikiwa ni zaidi ya Sh 129 milioni na mtu alitumia Akili Bandia (AI) kujifanya Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Tesla Elon Musk.

Wakati akifanyiwa mahojiano na vyombo vya habari nchini humo mwanadada huyo alieleza kuwa alikutana na tapeli huyo kupitia mtandao wa Instagram Julai 2023, ambapo walipeana namba na kuanza kuwasiliana ndipo baadaye akamuibia kiasi hicho cha pesa kilichokuwa kwenye akaunti yake.

Aidha kwa mujibu wa wanateknolojia walidai kuwa tapeli huyo alitumia Akili Bandia (AI) kutengeneza kitambulisho, video call za uongo na picha feki alizokuwa akimtumia ambazo zilifanya mwanadada huyo amuamini na kuingia naye kwenye mahusiano.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags