Cowboy Carter  ndiyo jina la albumu ya Beyonce

Cowboy Carter ndiyo jina la albumu ya Beyonce


Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Beyonce tayari amefichua jina la album yake mpya ambayo inatarajiwa kuachiwa mwishoni mwa mwezi huu aliyoipa jina la ‘Cowboy Carter’.

Beyonce ameweka wazi taarifa hiyo kupitia tovuti yake rasmi na mtandao wake wa Instagram. Hii itakuwa albamu ya nane kwa Queen Bey pia ni mwendelezo wa albamu ya Renaissance (Act I) ya mwaka 2022.

Kwa mujibu ya maelezo ya Beyonce wakati ametoa albumu ya Renaissance aliweka wazi kuwa albumu hiyo itakuwa na sehemu tatu hivyo basi (Act II: Cowboy Carter) ni sehemu ya pili ya Renaissance.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags