Chuo kikuu cha Yale chaanzisha somo kumsoma Beyonce

Chuo kikuu cha Yale chaanzisha somo kumsoma Beyonce

Na Masoud Kofii

Chuo Kikuu cha Yale kilichopo Marekani kimeanzisha mafunzo ya siasa na utamaduni huku kikitumia album za Beyonce kufundishia.

Albamu hizo ni kama vile Into Lemonde, Renaissance na Cowboy Carter ambayo inatajwa kuwa na grammy nyingi zaidi. Mafunzo hayo yatatolewa kwa ajili ya kumsoma Beyonce na kuwaruhusu wanafunzi kuchimba zaidi ustadi wa kisanii kutoka kwa nyota huyo wa kimataifa ambaye amekuwa na ushawishi kwenye muziki, siasa na utamaduni.

Mafunzo hayo yatafundishwa na mwalimu Darphine Brooks ambaye alianzisha kikundi cha Yales Black Sound & the archieve Working Group ikiwa ni jumuiya ya kitivo cha wanafunzi wanaofanya kazi kuchunguza aina mbalimbali za kumbukumbu za sauti za watu weusi ambazo hazijatumiwa

Brooks aliuambia mtandao wa Marekani NBC News kwamba mafunzo hayo yamekuwa yakifanya kazi kwa miaka mingi, kufuatia darasa la awali alilofundisha katika Chuo Kikuu cha Princeton lililopewa jina la "Black Women And Popular Music Culture".

Pia Brooks alisema hii itakuwa fursa yake ya kwanza kutoa kozi nzima kupitia kazi alizowahi kufanya Beyonce.

"Ninatazamia kuchunguza kazi yake na kuzingatia mambo mengine kama kumbukumbu za kihistoria, siasa za wanawake weusi, siasa za ukombozi wa watu weusi na kozi ya falsafa katika muongo uliopita,"aliiambia NBC kupitia barua pepe

Miaka ya 2010 Chuo Kikuu cha Rutger kilianzisha kozi ya Beyonce ikihusiana na Siasa lakini pia chuo kikuu cha "Illnois" cha Chicago kiliongeza kozi ya Beyonce ikiwa na lengo la kutazamia zaidi mtazamo wa Kifeminist na US Black Womanhood, Chuo kikuu cha Cornellnpia kimetoa matoleo ya kozi yake ya Beyonce Nation, ambayo inatoa historia ya kazi yake pamoja na athari zake kwenye harakati za kisiasa na ufeministi.

Vyuo vikuu vingine vilivyotoa kozi zinazofanana na za Beyonce ni pamoja na Chuo Kikuu cha Texas huko San Antonio, Chuo Kikuu cha Jimbo la California Polytechnic, na Chuo Kikuu cha Jimbo la Arizona.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post