Christian Bella afunguka alivyokata tamaa, Kurudi Congo

Christian Bella afunguka alivyokata tamaa, Kurudi Congo

Mwanamuziki #ChristianBella amesema kuna wakati alitaka kukata tamaa na kutaka kurejea nchini Congo baada ya mambo yake kuwa magumu Tanzania.

Msanii huyu ameeleza kuwa mwanzoni alipoanza muziki Tanzania mambo yalikuwa magumu sana kwake kwa sababu alikuwa anajisimamia mwenyewe na hakutaka mkataba wowote wa kusimamiwa kimuziki.

Hata hivyo amesema kuwa wimbo wake wa ‘Yako wapi mapenzi’ uliotoka mwaka 2014, ndiyo ulikuwa karata yake ya mwisho kujaribu upepo na ndiyo Project iliyompa mafanikio na kuinua matumaini yake ya kuendeleza muziki wake akiwa Bongo.

Msanii huyo wa Congo ambaye kumekuwa nyumbani anafanya kazi zake za muziki bongo amekuwa akifanya vizuri na ngoma zake kama vile 'Umebadilika', 'Mama' ,'Only you' na kwa sasa ameachia ngoma iitwayo 'Tamu' ambayo ina siku mbili tangu itoke huku ndani amemshirikisha Fid Q.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags