Chris Brown aikataa pesa ya shabiki

Chris Brown aikataa pesa ya shabiki

Mwanamuziki wa Marekani #ChrisBrown, ameripotiwa kurudisha pesa ya shabiki ambaye aliitoa kama malipo ili akutane na msanii huyo na kupiga naye picha.

Shabiki huyo wa kike mwenye ulemavu wa miguu alilipa dola 1,000 sawa na Sh 3 milioni kwa ajili ya kumuona na kupiga picha  na  nyota huyo wakati wa Tour yake ya 11 ‘Meet & Greet’ nchini humo.

Hata hivyo Breezy baada ya kuonana na mwanadada huyo uso kwa uso alimrudishia pesa yake pamoja na kumuongeza dola elfu 10 ikiwa ni sawa na Sh 26 milioni.

Chris Brown mwenye umri wa miaka 35 kila mwaka amekuwa akiandaa tour hiyo ya ‘Meet & Greet’ kwa ajili ya kuonana na mashabiki wake katika maeneo mbalimbali nchini humo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post