Chris brown aifanyia fitina show ya Quavo

Chris brown aifanyia fitina show ya Quavo

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani Chris Brown amedaiwa  kuwa alinunua viti vyote vya mbele kwenye moja ya show ya hasimu wake Quavo ili msanii huyo aonekane hajajaza ukimbi.

Kupitia video zinazosambaa mitandaoni zikionyesha viti vingi vya mbele havina watu katika moja ya show za Quavo zimesababisha mashabiki kuamini huenda ni kweli Brown ndiyo amefanya kitendo hicho kilicho sababisha mashabiki wengi wakose tiketi za kuingia katika ukumbi huo.

Wiki kadhaa zilizopita wawili hao wamekuwa katika muendelezo wa bifu lao ambapo kila mmoja alikuwa akitoa ngoma kwa ajili ya 'kumchana' mwenzake.

Bifu la Quavo na Brown lilianza mwaka 2017 baada ya Quavo kudaiwa kutoka kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Brown aitwaye Karrueche Tan.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags