Chini ya miaka 16 wapigwa marufuku kujihusisha na mitandao

Chini ya miaka 16 wapigwa marufuku kujihusisha na mitandao

Gavana wa mji wa Florida, nchini Marekani #RonDeSantis ametia saini mswaada wa sheria ya mitandao ya kijamii nchini humo jana Jumatatu kupiga marufuku watoto walio chini ya umri wa miaka 14 hadi 16 kujihusisha na mitandao ya kijamii.

Mbali na kizuizi hicho kwa vijana kutumia mitandao ya kijamii, sheria inayojulikana kama HB 3, pia inahitaji uthibitishaji wa umri kwa yeyote anayetaka kutembelea baadhi ya tovuti za falagha nchini humo.

Huku lengo kuu likitajwa kulinda watoto na mambo yasio faa yanayo pelekea kuporomoka kwa maadili na kupunguza magenge ya uhalifu nchini humo, Sheria hiyo inayotarajiwa kuanza kutumika Januari 1 2025.

Hata hivyo umoja wa wamiliki wa mitandao hiyo #NetChoice, ambao ni Meta, Google, X na TikTok, wamekuwa wakipinga mswaada huo huku #NetChoice ikituma ujumbe kupitia mtandao wa X kwamba uzuizi huo wa kutii sheria utahatarisha falagha za watu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags