Chidi adai kutopata kitu baada ya kufanya ngoma na Diamond

Chidi adai kutopata kitu baada ya kufanya ngoma na Diamond

Mwanamuziki wa Hip-hop nchini, #ChidiBenz amefungukua na kudai kuwa hakupata kitu baada ya #DiamondPlatnumz kuingiza mstari kwenye wimbo wake mpya uitwao ‘Tunaishi nao’, uliotoka miezi miwili iliyopita.

Chidi ameeleza kuwa pamoja na kuahidiwa vitu vingi ikiwemo kufanya promo na msanii huyo baada ya kufanya wimbo huo lakini hadi wimbo umetoka hajapata hata mia na hajafanya video ya wimbo huo mpaka sasa.

Hata hivyo amedai kuwa kabla wimbo huo kutoka Diamond alienda kwa #S2Kizzy na kuingiza mstari bila ruhusa yake, lakini hakuona kama kuna shida baada ya kukutana na msanii huyo na kumueeleza lengo la kufanya wimbo huo kwa pamoja.

Cc #Shajara

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags