Chanzo cha anguko la Ray C, awataja watoto wa 2000

Chanzo cha anguko la Ray C, awataja watoto wa 2000

Ikiwa ni mwendelezo wa historia ya mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva nchini, Rehema Chalamila maarufu Ray C kuhusu maisha yake, sasa ameeleza chanzo cha anguko lake lililopelekea kupoteza mwelekeo wa maisha huku akiwataja watoto wa 2000.

Kupitia ukurasa wa YouTube wa Ray C ame-share video akieleza kuwa alipoteza mwelekeo wa maisha kutokana na kampani ya watu aliyokuwa nao ambao ndio walimponza mpaka kuingia katika uraibu wa madawa.

“Nilizungukwa na watu wengi nilikuwa sijui yupi mbaya yupi mzuri na kipindi kile nilikuwa mdogo harafu napenda kampani na ndio maana hii kitu nataka kuongelea leo kwa sababu mimi kampani na kudate na watu nisio wajua vizuri ndio yaliyonifikisha nilipofika.

Anguko langu walikuwa ni wale wale watu ambao ni mpenzi wangu , marafiki na watu wangu wa karibu, niliwakaribisha kwenye maisha yangu kwa moyo mmoja ndio waliyoniponza kwahiyo nataka kuiongelea hii kitu kwa sababu nilikuwa ni mtu wa kushindwa kusema no, nilikuwa naamini sana watu na kutaka kujaribu kila kitu.

Na hicho ndio maana nataka kuongea kitu kilicho nitokea mimi ndio nakiona sasa hivi kwa watoto wa watoto 2000 kwa sababu ‘mnaspidi’ kilichoniponza mimi ni kiherehere na kujaribu kila kitu ambacho watoto wa 2000 ndio wanacho wanataka kujaribu kila kitu kufika club, kuvuta shisha na kunywa pombe hivi vyote ndio viliniponza mimi” amesema Ray C






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags