Chadema yaanza kupokea ruzuku
Kauli hiyo ameitoa Makamu mwenyekiti wa chama hicho ambapo hii ni mara ya kwanza kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kukiri kupokea ruzuku tangu kilipogoma kuichukua baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.
Aidha Tundu Lisu, amesema “Tumepokea sehemu tu ya pesa hizo na kiasi kilichosalia tutapewa siku za usoni. Tumeamua kuichukua kwasababu ya ahadi ya maridhiano yanayoendelea".
Hata hivyo Ruzuku hiyo inayokadiriwa kuwa zaidi ya Tsh. Milioni 110 waliigomea baada ya kukataa Matokeo ya Uchaguzi na Mazao yake
Leave a Reply