Chadema kuanza mikutano ya hadhara Desemba 2022

Chadema kuanza mikutano ya hadhara Desemba 2022

Msimamo huo umetangazwa Wilayani Sengerema na Mjumbe wa Kamati Kuu, John Heche kwa maelezo kuwa suala hilo ni Haki yao Kikatiba

Heche amesema “Ndani ya mwezi mmoja ujao tutatangaza ratiba na kuanza Mikutano ya Hadhara, mwaka 2022 hautaisha bila CHADEMA kufanya mikutano ambayo ni Haki ya Kikatiba na Kisheria kwa Vyama vyote vya Siasa”

Tangazo la CHADEMA limekuja kukiwa na vikao kadhaa vya Wadau wa Siasa kutafuta namna bora ya kuendesha shughuli zao ikiwemo Mikutano ya Hadhara iliyozuiwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya 5, Hayati John Magufuli Mei, 2016.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post