CEO wa Apple alitumia pombe kupata wafanyakazi

CEO wa Apple alitumia pombe kupata wafanyakazi

Inadaiwa mara nyingi watu huongea ukweli pindi wakiwa na hasira au wamelewa, kutokana na dhana hiyo aliyekuwa mmiliki na muanzilishi wa kampuni ya Apple, Steve Jobs kutoka nchini Marekani, aliitumia kwa ajili ya kupata wafanyakazi waaminifu.

Aprili 1, 1976 wakati kampuni ya Apple imeanzishwa ili kupata wafanyakazi Steve alitumia njia iliyofahamika kama ‘Beer Test’ ambayo aliwanywesha pombe waliokuwa wakiomba kazi kabla ya kuwafanyia interview.

Inaelezwa kuwa alikuwa anawachukua wote waliotuma maombi ya kazi na kuwapeleka matembezini kisha kuwanunulia pombe. Lengo lilikuwa ni kumjua vizuri mtu anayetarajia kumuajiri katika kampuni hiyo kwa sababu watu wakilewa hufunguka mengi.

Steve alifariki dunia mwaka 2011 katika mji wa Calfonia nchini humo akiwa na umri wa miaka 56.

Kwa unavyojijua unadhani ungetoboa kwenye interview?
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags