CEO Adidas amsifu Kanye West, Amtetea si mtu mbaya ni mtu mwema

CEO Adidas amsifu Kanye West, Amtetea si mtu mbaya ni mtu mwema

Mkurugenzi Mtendaji wa Adidas Bjorn Gulden, hatimaye akiwa kwenye podcast ya “In Good Company”, amtetea Kanye West kwa mara ya kwanza  tangu Adidas isitishe ushirikino wake na Kanye Oktoba mwaka jana, kutokana na kauli za chuki na upinzani alizokuwa akizitoa Kanye  kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Wayahudi.

Adidas ililazimika kusitisha ushirikiano wao kwa kudai kuwa hawavumilii chuki ya aina yoyote, hivyo kwa kauli za Kanye ni kukiuka maadili ya kampuni.

 Licha ya hayo yote hatimaye CEO wa kampuni hiyo ameeleza kuwa kashfa zilizotokea kwa Kanye zimegharimu kupoteza mamilioni ya pesa kwenye mauzo Adidas, lakini baada ya kusema hayo Bjorn amedai kuwa hadhani kama kauli za Kanye alizitoa kwa kumaanisha, kwani mwanamuziki huyo siyo mtu mbaya ni mtu mwema.

Hakuishia hapo na kusema kuwa anamsifu Kanye West kwa muziki anaofanya na ubunifu mbalimbali anaoendelea kuuonesha duniani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags