CCM yaijia juu TFS madai ya kuwapiga wananchi Ushetu

CCM yaijia juu TFS madai ya kuwapiga wananchi Ushetu

Chama cha Mapinduzi (CCM), imeijia juu Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwa madai ya kupiga wananchi wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga hadi kuwavunja miguu kwa kisingizo cha kuwakamata na mkaa ama kuwabambizikia kesi zizizo na msingi.

Akizungumza hayo juzi jimbo humo ,Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,Shaka Hamdu Shaka alisema Chama chao kinalaani vikali tabia hiyo inayofanywa na watu wa Mamlaka hiyo.

"Kibaya zaidi wanapowafikisha watuhumiwa polisi, hawawapeleki hata mahakamani wanatoleshwa faini ambazo hazina hata stakabadhi, niwakikishie wananchi Serikali CCM inayongozwa na Rais Samia haitavumilia jambo hili tunasimama upande wenu, kuweni na amani endeleni kutiii sheria bila shuruti" alisema


Alisema ni vema wakala hao wakatoa elimu ya Msingi na taratibun kwa wananchi ili waweze kujua na sio kuwadhalilisha vijana hao kwani wanaweza kutii Sheria bila shuruti."CCM haiwezi kukubali hali hii ya vijana kudhalilishwa,tukitoka hapa nitampigia simu Waziri mwenye dhamana na kuzungumza nae juu ya hili suala waache mara moja kuwadhalilisha vijana,"alisema na kuongeza

"CCM haitakubali kuona wananchi kwenye maeneo ya hifadhi ya misitu wakiishi kama vile wao ni wakimbizi katika nchi yao. TFS acheni uonevu na unyanyasaji wa wananchi wanaopakana na misitu hususan hapa Jimbo la Ushetu,"alisema

Alisema Chama kitaelekeza serikali kuweka utaratibu mzuri wa kuheshimu vijana ili nao wawaheshimu vizuri na kuacha kuwavunja miguu na kuwadhalilisha.

Aidha Shaka alisema anatarajia kuwasiliana na Inspekta Jenerali wa Polisi,Saimon Sirro juu ya tabia ya baadhi ya Askari Polisi katika jimbo la Ushetu
kupambikiziwa wananchi kesi za kukamatwa na bangi hususani kwa vijana na wanawake ambavyo vinavyofanywa na baadhi ya askari wasio waaminifu wa mkoa huo.

"Chama Cha Mapinduzi tutazungumza na IGP leo hii jicho lake liangalie wilaya ya Kahama haiwezekani wananchi wako kwenye nchi huru leo hii wakafanywa wanaishi kama wakimbizi kwa vitu vya kusingiziana na kubambikiziana kesi kubwa na zito,"alisema Shaka

"Chama hakikubaliani na hili hata kidogo na wala hakiridhishwi kwa utendaji huo wa baadhi ya Askari nitamtafuta IGP na kuzungumza nae juu ya hili kwani wanawake na vijana wanachukuliwa mali zao na kuharibiwa na hawa Askari,"alisema

Shaka alisema Chama kipo imara na hakikubaliani na Tabia hizo hivyo wanataka kuzimaliza iwe mwanzo na mwisho."Tumekuwa tukihubiri amani ,umoja na mshikamano wakati wote lazima wananchi wawe na imani na vyombo vyao vya dola na lazima wote twende pamoja katika safari iliyokusudiwa, "alisema

Wakati huo huo Shaka alisema suala la ushindi katika Jimbo la Ushetu halina mjadala wanashinda kwa sababu wamekuwa wakitatua changamoto za wananchi hususani kipindi hiki cha awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Alisema tayari mkoa wa Shinyanga unamradi Mkubwa wa maji safi na salama ambao upo katika hatua ya upembuzi yakinifu na upo katika hatua nzuri kutoka ziwa Victoria.

"Rais Samia kawaletea Milioni 400 kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo la upembuzi yakinifu ili kuhakikisha jimbo hilo maji safi na salama yanapatikana kwa uhakika na tatizo la maji kuwa la historia kwa muda mfupi ujao,"alisema na kuongeza

"Tayari Bilioni 6 zimefika kwa Mamlaka ya maji vijijini kwa jimbo hili kuhakikisha miundombinu ya maji inatandikwa kuwafikia wananchi,"alisema Shaka

Alisema mbali na suala la maji,serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia imetoa Bilioni 72 kwaajili ya ujenzi wa barabara na ukarabati Stendi za mabasi na madampo.

Shaka alisema upande wa elimu kwa mkoa wa Shinyanga Rais Samia kila mwezi anatoa sh.Milioni 591 kwaajili ya kuwalipia watoto ili wapate elimu bure bila malipo."CCM inakazi moja tu kuleta maendeleo katika jimbo la Ushetu ambapo kwenye sekta ya afya Milioni 750 za tozo ya miamala zimeletwa katika mkoa huo kwa ajili ya afya mkoani humo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags