Cassie azidi kumkaanga Diddy

Cassie azidi kumkaanga Diddy

Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Hip-hop Diddy, Cassie ameripotiwa kushirikiana na vyombo vya dola katika uchunguzi wa kesi ya biashara ya ngono inayomkabili Combs.

Kwa mujibu wa Tmz imeeleza kuwa wapo baadhi ya watu wa karibu wanatoa ushirikiano kwa mamlaka hiyo lakini mwanamuziki Cassie ndiye kinara huku akidhaniwa kuwa alianza kutoa ushirikiano kwa mamlaka hizo za uchunguzi toka nyumba za Diddy hazijapigwa msako.

Ikumbukwe kuwa Cassie ndiye mwanamke wa kwanza kufungua kesi Diddy ya unyanyasaji wa kingono, kesi ambayo ilifunguliwa Novemba 16, mwaka jana.

Lakini pia baada ya kufungua kesi hiyo mahakamani wawili hao siku iliyofuata Novemba 17 walifikia makubaliano ya kusuluhisha suala hilo kwa Amani bila kufichua maelezo zaidi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags