Casanova akabiliwa na kesi ya mauaji

Casanova akabiliwa na kesi ya mauaji

Rapa kutoka nchini Marekani  Casanova  mwishoni mwa mwaka 2020 alikamatwa kwa Tuhuma za kujihusisha na genge la kihalifu liitwalo, Untouchable Gorilla Stone Nation, Ambapo Shirika la Kijasusi nchini Marekani (FBI) lilitoa taarifa kupitia twitter.

Taarifa hiyo  ambayo ilikuwa ikiuelezea Umma kuwa inawashikilia member 17 wa genge hilo kwa makosa ya kujihusisha na biashara haramu, mauaji, dawa za kulevya na makosa ya kumiliki silaha kinyume cha sheria

Casanova Pamoja na Genge hilo la kihalifu (Untouchable Gorilla) wanatajwa kuwa walihusika katika mauaji ya kijana mwenye umri wa miaka 15 huko Poughkeepsie, sasa Rapa huyo ameshtakiwa kwa kosa la kujaribu kufanya Mauaji.

Tukio hilo la kujaribu kufanya mauaji linaripotiwa kuwa lilitokea Oktoba 24, 2020 mjini Miami Club alipogombana na mwanachama wa Genge hasimu na kumshambulia kwa Risasi Tumboni.

Kwa mujibu wa ofisi ya mwanasheria Mkuu mjini New York, Casanova pamoja na wenzake wakikutwa na hatia hivyo watakutana na kifungo cha maisha gerezani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags