Carragher ampa maua yake Emery

Carragher ampa maua yake Emery

Mwanasoka wa zamani #JamieCarragher amemtaja kocha wa ‘klabu’ ya #AstonVilla, #UnaiEmery kuwa ndiye kocha bora zaidi katika msimu huu kwenye ‘ligi kuu ya #England na kuwapiga chini ‘makocha’ mashuhuri kama #JurgenKlopp na #PepGuardiola.

Carragher akizungumza na tovuti ya Sky Sport New amempa maua yake Kocha huyo kutokana na ubora wake wakukiongoza vizuri kikosi hicho msimu huu.

Kocha huyo raia wa Uhispania alijiunga na Aston Villa akitokea #Villarreal, Oktoba 2022, pia akiwa Aston Villa amefanikiwa kuimaliza nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu ya England na kupata tiketi ya kwenda kushiriki michuano Ulaya.

Hata hivyo ameendelea kuwasha moto msimu huu, ambapo kwasasa ameiwezesha timu hiyo kufika nusu fainali ya Europa Conference League huku kukiwa  na  uwezekano wa kufuzu kucheza ‘Ligi’ ya Mabingwa #Ulaya msimu ujao kutokana na kushika nafasi ya nne kwenye ‘ligi’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post