Kipa wa Simba, Moussa Camara amezungumzia ubora wa ukuta wa timu hiyo unaongozwa na Fondoh Che Malone na Abdulrazack Mohamed Hamza kama sehemu ya kufanya kwake vizuri katika michezo mitano iliyopita katika Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Afrika ambapo ameruhusu bao moja tu.
Camara aliyecheza kwa umahiri mkubwa katika mchezo wa ligi dhidi ya Azam uliopigwa visiwani Zanzibar na Simba kushinda mabao 2-0, huku akichaguliwa Nyota wa Mchezo, alisema hakuna maajabu kwake zaidi ya ushirikiano mzuri ambao amekuwa akiupata kwa wachezaji wenzake.
Kipa huyo aliyasema katika mahojiano maalumu na mtandao wa Simba na kusema “Najisikia vizuri sana. Tumefanya kazi kubwa kwa sababu ilikuwa mechi muhimu na tumefanya kila juhudi kushinda. Nafurahi sana kwa jinsi tulivyofanikisha ushindi huu katika mchezo huu mkubwa.”
“Tumekuwa tukifanya kazi kwa ushirikiano, Malone na Hamza wamekuwa na mchango mkubwa na hata Chamou Karaboue, Kapombe, Tshabalala na timu kwa jumla bila wao ni ngumu kucheza bila ya kuruhusu bao, naamini tutaendelea kuwa bora zaidi.”
Leave a Reply