Calm Down yaendelea kuwapaisha Rema na Serena Gomez

Calm Down yaendelea kuwapaisha Rema na Serena Gomez

Kutokana na ngoma ya Rema na Serena Gomez kufanya vizuri duniani kote hatimaye wawili hao wameshinda Tuzo ya MTV katika kipengele cha wimbo bora wa Afro Beats kupitia wimbo wao wa “Calm Down Remix”.

Tuzo hizo zimetolewa usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Prudential Center, New Jersey nchini Marekani.

Hata hivyo baada ya kukabidhiwa tuzo Rema alimtaka Serena azungumze chochote, mwanadada huyo alieleza hisia zake kwa kumshukuru Rema kukubali kufanya naye  remix.

 Pia Serena akawashukuru wote kwa kusikiliza na ku-stream wimbo huo, mwisho kabisa akawashukuru wanaigeria wote kwa ‘kusapoti’ wimbo huo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags