Busu la Bieber kwa Jaden Smith lazua gumzo

Busu la Bieber kwa Jaden Smith lazua gumzo

Ikiwa zimepita siku chache tangu tamasha la muziki la Coachella kufanyika, limezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii, baada ya mwanamuziki Justin Bieber kuonekana akimbusu Jaden Smith shavuni.

Gumzo hilo limezuka baada ya kipande cha video kusambaa kwenye  mitandao ya kijamii kikimuonesha Bieber akimsalimia Jaden tofauti na watu wengine kwa kumkumbatia na kumbusu shavuni.

Ikumbukwe kuwa wawili hao walianza urafiki toka mwaka 2010, baada ya kufanya ‘kolabo’ ya wimbo wa (Never Say Never) uliotumika katika filamu ya ‘Karate Kid’ ambayo Jaden alikuwa muhusika mkuu.

Tamasha la Coachella lilibamba zaidi baada ya Justin Bieber kuwapandisha wakali wa Afrobeat kutoka Nigeria ambao ni Tems na Wizkid ambapo walitumbuiza kwa pamoja ngoma ya ‘Essence’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags