Burna Boy kuwaweka wanablogu kikaangoni

Burna Boy kuwaweka wanablogu kikaangoni

Ikiwa ni wiki chache tangu mkali wa Afrobeat Burna Boy kutaka kuwalipa pesa waandishi wa blog nchini Nigeria ili waache kuandika habari zake, hatimaye mwanamuziki huyo amedai kuwa anampango wakutafuta mawakili 100 kwa ajili ya kushuhurika na wana-bog wanaoendelea kuandika habari zake.

Burna Boy ameweka wazi suala hilo kupitia ukurasa wake wa X kwa kueleza kuwa pesa alizopanga kuwalipa wana-blog ili waache kuandika habari zake, sasa anawaza kuwapa mawakili 100 ili kushughulikia jambo hilo.

Burn Boy anaendelea kufanya vizuri katika muziki wa Afrobeat ambapo anatamba na ngoma zake kama ‘Last Last’ ‘For My Hand’ aliomshirikisha Ed Sheeran, ‘It's Plenty’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags