Burna Boy ana jambo lake hivi karibuni

Burna Boy ana jambo lake hivi karibuni

Mkali wa afrobeat kutoka Nigeria, Burna Boy amedai kuwa ngoma yake ijayo ndio itakuwa ngoma bora kushinda ngoma zote zilizotoka mwaka huu.

Mwanamuziki huyo ameyasema hayo kwenye mahojiano yake wakati alipokuwa kwenye onesho la mitindo la ‘Paris Fashion Week’ ambapo aliweka wazi kuwa kuna nyimbo ameirekodi siku mbili zilizopita huku akiamini kuwa ndio itakuwa bora kushinda zote.

Kwa sasa Burna Boy anatamba na ngoma ya ‘Tshwala Bam Remix’ aliyoshirikishwa na TitoM, Yuppe ambapo mpaka kufikia sasa ina zaidi ya watazamaji milioni 7.9 kupitia mtandao wa YouTube.

Katika onesho hilo la mitindo lililofanyika Jana jijini Paris nchini Ufarasa mwanamuziki huyo alifanikiwa kutumbuiza ngoma zake mbalimbali ikiwemo ‘Tshwala Bam Remix’ kwenye Party iliyoandaliwa na ‘Paris Fashion Week’.

Mastaa wengine ambao walifanikiwa kuhudhuria katika maonesho hayo ni Rema, Wizkid, Maluma, Swae Lee na wengineo.
.
.
.
#MwananchScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags