Burna boy afichua thamani yake, Ni zaidi ya sh 55 bilioni

Burna boy afichua thamani yake, Ni zaidi ya sh 55 bilioni

Mwanamuziki kutoka Nigeria Burna Boy ameweka wazi kuwa thamani yake ni zaidi ya tsh 55 bilioni kama mtandao wa google unavyoeleza.

Kwa sasa ukingia katika mtando wa google na kutafuta thamani ya mwanamuziki huyo utaeleza kuwa ni ‘dola’ 22 milioni ambayo ni zaidi ya tsh 55 bilioni, lakini Burna amekanusha na kudai kuwa thamani yake ni zaidi ya kiwango cha pesa wanachoeleza google.

Burna Boy amefichua hayo katika mahojiano yake na chombo cha habari cha Marekani Complex, kwa akidai kuwa kiwango hicho sio sahihi lakini hakuweka wazi kiwango sahihi cha thamani yake, huku akisema kuwa kikubwa anachoshukuru ni anauwezo wa kuhudumia familia yake.

Mkali huyo kutoka Nigeria akaongezea kwa kusema kuwa wakati akiwa mtoto alikuwa akimwambia mama yake kuwa siku moja atamnunulia nyumba na gari, lakini yote kwa sasa anaweza kuyafanya.

.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags