Burna Boy afanya show ya kibabe, Ajaza uwanja

Burna Boy afanya show ya kibabe, Ajaza uwanja

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Burna Boy anazidi kuweka historia katika mataifa mbalimbali ambapo usiku wa kuamkia leo amefanya show iliyo hudhuriwa na watu 80,000 katika Uwanja wa London Stadium nchini Ungereza.

Inaelezwa nyomi ya mashabiki walifika mapema kushuhudia burudani ya staa huyo wa Nigeria jana Jumamosi katika uwanja huo wa mpira nchini humo.

Aidha baada ya onesho hilo  Burna Boy alitoa shukrani zake kwa mashabiki wote waliofika kwenye tamasha lake lililotikisa jiji zima la London.

Hata hivyo, kwa msanii huyo imekuwa ni kawaida show zake kufurika watu wengi hali ambayo inazidi kumpa umaarufu katika muziki wake ulimwenguni.

Mbali na hayo #Harmonize ameonesha kushangazwa na show hiyo ya Burna Boy akidai kuwa  msanii huyo amebadilika tofauti na zamani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags