Bukta ya bondia Muhammad kupigwa mnada

Bukta ya bondia Muhammad kupigwa mnada

Bukta ya bondia wa zamani wa ngumi za kulipwa Muhammad Ali maarufu kama ‘The Greatest’ aliyoivaa katika pambano lake na Joe Frazier inatarajiwa kuuzwa kiasi cha dola 6 milioni ikiwa ni zaidi ya Sh 15 bilioni.

Bukta hiyo nyeupe iliyosainiwa na Ali mwenyewe itauzwa katika mnada utakaofanyika Sotheby’s jijini New York, Ijumaa April 12, na hii siyo mara ya kwanza kwa bukta hiyo kuuzwa kwani mwaka 2012 iliwahi kuuzwa kwa dola 150,000.

Ikumbukwe kuwa Muhammad Ali alimchakaza na Joe Frazier katika pambano lililojulikana kama ‘Thrilla in Manila’ lilichezwa Oktoba mwaka 1975 mji mkuu wa Ufilipino.

Ali, mmoja wa magwiji wa mchezo huo alifariki Juni 2016 akiwa na umri wa miaka 74 baada ya kuishi na ugonjwa wa Parkinson kwa muda mrefu, huku Frazier alifariki mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 67.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post