Bruno Gomez azua gumzo mitandaoni

Bruno Gomez azua gumzo mitandaoni

Kiungo wa Singida BS, Bruno Gomez alizua gumzo zaidi jana baada ya kwenda kwenye benchi la Yanga na kuwasalimia wachezaji wa akiba pamoja na makocha wao kabla mchezo haujaanza.

Pia baada ya mchezo kumalizika alionekana akizungumza mara kwa mara na viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo, hali ambayo iliwafanya wengi waamini kuwa anaweza kujiunga na timu hiyo ya Jangwani mwishoni mwa msimu huu.

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga imeondoka na alama tatu ugenini baada ya kuwachapa wenyeji wao Singida Big Stars kwa mabao 2-0 kwenye mchezo uliomalizika katika Uwanja wa CCM Liti Mkoani Singida.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags