Bruce Africa aeleza Master J alivyomliza

Bruce Africa aeleza Master J alivyomliza

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Bruce amesema wakati yupo BSS, alikuwa anaumizwa na majibu ya Master J, lakini hadi sasa wapo sawa kwani anaamini alikuwa anamjenga na si vinginevyo.

Bruce anaeleza ubaya ulikuwa Master anavyotoa 'komenti' na inavyomfikia, hasa kuambiwa hamna kitu anasema kama angekuwa legelege angekata tamaa, lakini kwakuwa alijua anachotaka hivyo haikumvunja moyo.

"Ilikuwa inaniumiza sana, hasa kwenye kile kipindi cha ‘All Stars’, ilifika muda nikawa nalia nikifika nyumbani, japo pale mbele nilikuwa nacheka sioneshi ila nikifika nyumbani nalia, yaani muziki nautegemea halafu nakataliwa mbele za watu hadi kuna kipindi nilifikiria kwani nilizaliwa ili nishindanage, ila naamini ilikuwa ni changamoto tu,” anasema Bruce






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags