Boris: Putin alitishia kuniua

Boris: Putin alitishia kuniua

 Taarifa kutoka Uingereza ambapo aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amefichua kwamba Rais wa Urusi, Vladmir Putin alitishia kumuua endapo angeendelea na mpango wake wa kuisaidia Ukraine kabla nchi hiyo haijaivamia na kusababisha vita ambavyo mpaka sasa vinaendelea.

Boris ameyasema hayo wakati akihojiwa na Shirika la Habari la Uingereza, BBC ambapo ameeleza kuwa Putin alimpa vitisho hivyo, Februari 2022, muda mfupi baada ya Boris kurejea kutoka kwenye ziara yake nchini Ukraine na kuitaka Urusi iachane na mpango wa kuivamia Ukraine.

“Aliniambia, Boris sitaki kukuumiza lakini kwa kombora, itachukua dakika moja tu,” amenukuliwa Boris na kueleza kuwa, alipigiwa simu na Putin na kupewa vitisho hivyo baada ya kurejea kutoka Ukraine.

Alipewa vitisho hivyo, baada ya Boris kukutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky jijini Kyiv ambapo alimhakikishia kwamba Uingereza itaisaidia Ukraine endapo Urusi itaivamia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags