Bobi Wine awaonya wakenya juu ya pendekezo la kuondoa ukomo wa muhula wa urais nchini humo. Kiongozi huyo wa upinzani Uganda, amewataka Wakenya kuwa macho kwa kulinganisha hali ilivyo nchini Uganda ambako ukomo wa mihula ya rais iliondolewa na Rais Yoweri Museveni.
Bobi anatoa rai hiyo baada ya Mbunge wa Kenya Salah Yakub, kuibua mjadala aliposema muungano tawala utashinikiza marekebisho ya katiba ili kumaliza ukomo wa mihula na badala yake waweke umri wa miaka 75 kama ukomo wa rais kuongoza.
Hata hivyo, chama cha United Democratic Alliance (UDA) kimepuuzia mbali madai kwamba wabunge washirika wa chama hicho wanapanga kufuta ukomo wa mihula miwili ya urais.
“Kama chama tunasalia kuunga mkono ukomo wa mihula miwili ya urais na (hakuna) mijadala inayoendelea ya kuufuta,” alisema Johnson Muthama wa UDA.
Endapo marekebisho yakuzingatia umri yatafanyika Kenya, Rais William Ruto, mwenye umri wa miaka 55, ataweza kusalia madarakani kwa miaka 20.
Leave a Reply