Ocean builders na mpango kuzindua nyumba juu ya bahari

Ocean builders na mpango kuzindua nyumba juu ya bahari

Watu kuishi katika sehemu za kawaida kama nchikavu, katika misitu na sehemu nyingine ni jambo la kawaida lakini binadamu kuishi katikati ya maji inaweza ikawa inashangaza.

Kampuni ya Ocean Builders, iliyopo pwani ya Panama, Amerika ya kati inampango wa kuzindua makazi (nyumba) za kuishi watu, zilizojengwa juu ya bahari, mwaka 2024.

Nyumba hizo ambazo zilizopewa jina la ‘Sea living pod’ zitaruhusu kuishi watu wawili tu, huku mbunifu kutoka Uholanzi Koen Olthuis, Mhandisi Rüdiger Koch pamoja na Afisa Mkuu Mtendaji Grant Romundt walieleza kuwa wamebuni makazi hayo kama suluhisho kwa watu ambao watakosa makazi ya kuishi.


‘Living pod’ zitakua na chumba cha kulala, bwawa la kuogelea, sebule, jiko pamoja na bafu la viwango vya juu, huku nyumba hiyo ikigharimu kiasi cha dola 295,000 ambayo ni zaidi ya tsh 752 milioni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post