Aika Awafunda Wanawake Kuhusu Mahusiano

Aika Awafunda Wanawake Kuhusu Mahusiano

Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni mshirika wa kundi la muziki la Navykenzo, Aika amewashauri wasichana kutokuwa na matarajio makubwa kutoka kwa wanaume.

Aika ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa wanaume ni wenye hisia hulia na sio wakamilifu hivyo wasitegemee makubwa katika kutimiziwa matamanio yao.

"Warembo huenda mmepoteza miaka mingi ya kufurahia na kujenga uhusiano, kwa sababu ya matarajio yenu makubwa na ndoto zenu kuhusu mwanaume. Wanaume ni wenye hisia, hulia, si wakamilifu hawakuzaliwa na maarifa yote ya kuweza kutimiza mataminio yenu," amesema

Ameendelea kusema kuwa wasichana wasipoteze muda mwingi kutafuta mwanadamu mkamilifu kwani ni ngumu kumpata bali watu hurekebishana na kujengana.

"Msipoteze muda wenu mkitafuta mwanadamu mkamilifu atakaye waletea chai kitandani, maua kazini, au kuwasurprise kwa likizo, badala yake chukueni muda kujengana, kusaidiana, kufundishana uhusiano hujengwa kama nyumba sio muujiza," amesema Aika.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags